Matumizi ya Maigizo Kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia Katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenya
View/ Open
Publication Date
2019Author
8. Simbi, I., Wasike, M., Amukowa, D., & Masinde, E
Metadata
Show full item recordAbstract/ Overview
Utafiti huu ulilenga kuonyesha matumizi ya maigizo kama mbinu ya kufundisha
tamthilia; mfano wa Kigogo katika shule za upili, Kaunti ya Bungoma Kusini.
Ufundishaji wa somo lolote hujikita kwenye mawasiliano baina ya mwalimu na
mwanafunzi. Mbinu za kufundisha huwa viungo muhimu vya kufanikisha
mawasiliano haya. Mwalimu ana jukumu la kuteua mbinu mwafaka ya
kufundisha. Kuna mbinu mbalimbali mwalimu anaweza kutumia kufundisha
tamthilia. Utafiti huu umechagua maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia.
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza iwapo walimu wanatumia mbinu ya
maigizo kufundisha tamthilia na wanatumia kwa jinsi gani. Utafiti huu
uliongozwa na nadharia ya utendaji inayoshikilia kuwa matini ya kidrama
huwasilisha ujumbe vyema zaidi kupitia uigizaji wake katika jukwaa. Utafiti
ulilenga shule kumi na sita kati ya shule hamsini na mbili. Walimu
wanaofundisha Kiswahili kidato cha tatu na nne pamoja na wanafunzi wa kidato
cha tatu na nne ndio waliolengwa. Watafitiwa waliteuliwa kwa kutumia mbinu
ya utabakishaji, kinasibu na usampulishaji kimaksudi. Stadi ya utabakishaji
ilitumika kuainisha shule katika makundi matatu. Mbinu ya kimaksudi ilitumika
kuteua shule tatu za kaunti na walimu wanaofundisha kiswahili kidato cha tatu
na nne. Mbinu ya kinasibu ilitumika kuteua shule za kaunti ndogo, shule kumi
na mbili na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Wanafunzi kumi katika kila
kidato waliteuliwa, jumla ya wanafunzi mia tatu ishirini walitafitiwa. mbinu
zlizotumika kukusanya data zilikuwa hojaji, maswali ya usaili na uchunzaji.
Maswali ya usaili yalitumika kukusanya data kutoka kwa walimu. Data
ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia maelezo, asilimia, picha na
majedwali. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kuwa walimu 83% ndio walitumia
mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia ya Kigogo. Utafiti unapendekeza kuwa
mbinu za maigizo ambazo hazitumiki pia zitumike ili kuboresha ufundishaji.
Vile vile taasisi ya elimu kuandaa semina na warsha za kuwahamasisha walimu
kuhusu njia mbalimbali za kutumia maigizo kufundisha. Aidha kila shule iwe
na klabu cha maigizo ili kutumika katika ufundishaji wakati wowote.