Show simple item record

dc.contributor.author8. Simbi, I., Wasike, M., Amukowa, D., & Masinde, E
dc.date.accessioned2022-02-07T08:16:05Z
dc.date.available2022-02-07T08:16:05Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttps://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/4888
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuonyesha matumizi ya maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia; mfano wa Kigogo katika shule za upili, Kaunti ya Bungoma Kusini. Ufundishaji wa somo lolote hujikita kwenye mawasiliano baina ya mwalimu na mwanafunzi. Mbinu za kufundisha huwa viungo muhimu vya kufanikisha mawasiliano haya. Mwalimu ana jukumu la kuteua mbinu mwafaka ya kufundisha. Kuna mbinu mbalimbali mwalimu anaweza kutumia kufundisha tamthilia. Utafiti huu umechagua maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza iwapo walimu wanatumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia na wanatumia kwa jinsi gani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utendaji inayoshikilia kuwa matini ya kidrama huwasilisha ujumbe vyema zaidi kupitia uigizaji wake katika jukwaa. Utafiti ulilenga shule kumi na sita kati ya shule hamsini na mbili. Walimu wanaofundisha Kiswahili kidato cha tatu na nne pamoja na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne ndio waliolengwa. Watafitiwa waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya utabakishaji, kinasibu na usampulishaji kimaksudi. Stadi ya utabakishaji ilitumika kuainisha shule katika makundi matatu. Mbinu ya kimaksudi ilitumika kuteua shule tatu za kaunti na walimu wanaofundisha kiswahili kidato cha tatu na nne. Mbinu ya kinasibu ilitumika kuteua shule za kaunti ndogo, shule kumi na mbili na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Wanafunzi kumi katika kila kidato waliteuliwa, jumla ya wanafunzi mia tatu ishirini walitafitiwa. mbinu zlizotumika kukusanya data zilikuwa hojaji, maswali ya usaili na uchunzaji. Maswali ya usaili yalitumika kukusanya data kutoka kwa walimu. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia maelezo, asilimia, picha na majedwali. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kuwa walimu 83% ndio walitumia mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia ya Kigogo. Utafiti unapendekeza kuwa mbinu za maigizo ambazo hazitumiki pia zitumike ili kuboresha ufundishaji. Vile vile taasisi ya elimu kuandaa semina na warsha za kuwahamasisha walimu kuhusu njia mbalimbali za kutumia maigizo kufundisha. Aidha kila shule iwe na klabu cha maigizo ili kutumika katika ufundishaji wakati wowote.en_US
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studiesen_US
dc.subjectMaigizo, Tamthilia, Mbinu, Ufundishajien_US
dc.titleMatumizi ya Maigizo Kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia Katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenyaen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record