Show simple item record

dc.contributor.authorMUSAMALI, Charles Omukuba
dc.date.accessioned2021-05-07T08:49:00Z
dc.date.available2021-05-07T08:49:00Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.urihttps://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/3709
dc.description.abstractIKISIRI Matumizi ya mikakati mbalimbali ya kipragmatiki katika diskosi huweza kuzua utata katika kufasiri ujumbe ulionuiwa kumfikia msomaji au msikilizaji. Tamko la msemaji au mwandishi fulani huweza kufasiriwa na msikilizaji au msomaji kwa njia mbalimbali. Hali kama hii huibua maana mbalimbali za ujumbe mmoja ambapo mawasiliano hutatizika. Utafiti huu ulinuia kubaini jinsi mikakati ya kipragmatiki inavyodhihirika katika diskosi za uhifadhi wa misitu katika gazeti la Taifa Leo nchini Kenya. Vile vile utafiti huu ulinuia kuonyesha j insi mikakati hiyo inavyoathiri ufasiri wa ujumbe unaodhamiriwa na mwandishi hivyo basi kutatiza juhudi za serikali za kuhifadhi misitu. Malengo ya utafiti huu yalikuwa: Kubaini mikakati ya kipragmatiki inayotumiwa katika diskosi za uhifadhi wa misitu ili kupitisha ujumbe ulionuiwa na mwandishi, kujadili njia mbalimbali zinazotumiwa na umma kufasiri maana katika habari juu ya uhifadhi wa misitu na mwisho, kueleza athari ya ufasiri wa kipragmatiki wa habari juu ya uhifadhi wa misitu kwa shughuli za uhifadhi wa misitu. Nadharia ya kipragmatiki ya 'umaanishi wa kimaongezi' ya Grice ilituongoza katika utafiti huu. Data kuhusu mikakati mbalimbali ya kipragmatiki katika diskosi ya uhifadhi wa misitu ilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi wa yaliyomo ambapo nakala zote 36 za magazeti ya Taifa Leo ya mwaka baina ya 2008 na 2009 zilihusishwa. Mikakati mbalimbali ya kipragmatiki kama vile, matumizi ya jazanda,· kinaya, umaanisho, semi, vionyeshi na matumizi ya uongo ilibainishwa. Hojaji iliyotayarishwa na mtafiti kwa kuzingatia mada ya utafiti huu ilitumiwa kukusanya data kutoka kwa umma. Jumla ya watu wazima 50 wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaojua kusoma na kuandika kutoka katika eneo la Msitu wa Kakamega haswa kata za Lukusi, Ivihiga, Kambiri na Lubao waliokuwa wakihudhuria mabaraza ya chifu walijitokeza kuhojiwa. Wahojiwa hao walipokezwa hojaji ambapo walizijaza kwa kuzingatia maswali yaliyokuwa yameulizwa. Aidha utafiti huu ulidhihirisha kuwa matumizi ya kinaya na jazanda katika habari juu ya uhifadhi wa misitu ndiyo husababisha ufasiri uliopotoka wa kiwango cha juu zaidi-asilimia 64% na 42% mtawalia. Utafiti huu vilevile ulidhihirisha kuwa ufasiri wa kipragmatiki wa habari juu ya uhifadhi wa misitu na umma una athari hasi katika shughuli za uhifadhi wa misitu. Kutokana na matokeo ya utafiti huu mapendekezo yafuatayo yalitolewa: Uhariri wa habari zinazochapishwa katika gazeti la Taifa Leo juu ya uhifadhi wa misitu ufanywe kwa misingi ya kuhakikisha kuwa utata wa ufasiri wa habari unaotokana na kuwepo kwa mikakati ya kipragmatiki umepunguzwa kabisa kama sio kuondolewa.en_US
dc.publisherMaseno Universityen_US
dc.titleUfasiri Kipragmatiki Wa Diskosi Katika Gazeti La Taifa Leo Juu Ya Uhifadhi Wa Misitu Kenyaen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record