Show simple item record

dc.contributor.authorOdhong’, Joseph Ondiek
dc.contributor.authorAmukowa, Debora Nanyama
dc.contributor.authorAsiko, Beverlyne Ambuyo
dc.date.accessioned2023-11-08T17:01:51Z
dc.date.available2023-11-08T17:01:51Z
dc.date.issued2023-07-31
dc.identifier.issn2707-3475 online
dc.identifier.issn2707-3467 print
dc.identifier.urihttps://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5841
dc.descriptionhttps://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1345en_US
dc.description.abstractTakwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi mazingira wanamoishi. Tangu jadi wahakiki wamejitahidi kueleza vipi wahusika wazimu wametumika katika fasihi. Tahakiki za tamthilia za Shakespeare na za Kiingereza za karne ya ishirini zimeeleza namna na sababu za uumbaji wao. Katika riwaya za Kiswahili hakuna tahakiki zinazoshughulikia wahusika wazimu wala mitindo ya lugha inayowabainisha. Makala hii ilidhamiria kuchanganua mitindo ya lugha inayowabainisha wahusika wazimu katika kazi teule za Habwe. Uteuzi huu ulitokana na Habwe kusifiwa kuwa mwandishi wa fasihi ya kiongofu aliyetumia motifu ya wazimu katika riwaya zake (Gromov, 2018). Riwaya tano za Habwe: Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008), Fumbo La Maisha (2009), Safari ya Lamu (2011) na Kovu Moyoni (2014) ziliteuliwa kupitia usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zilikuwa na wahusika wazimu. Nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Bally (1909) ) na kuendelezwa na Thornborrow na Wareing (1998) iliteuliwa kwa ajili ya kazi hii. Muundo wa kiuchanganuzi umetumiwa. Data zilikusanywa kutumia kifaa cha kudondoa data kilichokuwa na vidokezo vya mitindo ya lugha inayotambulisha wahusika wazimu. Matini ya riwaya teule imesomwa kwa makini na vipengele mbalimbali, kurekodiwa. Kisha data imechanganuliwa, kufasiriwa na kuratibiwa kulingana na madhumuni ya utafiti. Matokeo yamewasillishwa kwa njia ya maelezo. Makala hii imedhihirisha jinsi mitindo ya lugha ilivyotumiwa kuwatambulisha wahusika wazimu.en_US
dc.publisherEASTAFRICAN NATURE& SCIENCE ORGANIZATIONen_US
dc.subjectMotifu, Wahusika wazimu, Mitindo, Uumbajien_US
dc.titleMitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habween_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record