Jinsi Mtindo Katika Ushairi Unavyofundishwa Katika Shule za Upili: Mfano wa Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini, Kaunti ya Busia, Kenya
View/ Open
Publication Date
2019Author
9. Mukoya, H., Wasike, M., Amukowa, D., & Masinde, E
Metadata
Show full item recordAbstract/ Overview
Makala hii inahusu jinsi ambavyo mtindo katika ushairi unavyofundishwa katika shule za upili nchini Kenya. Wasomi mbalimbali wametafiti kuhusiana na jinsi ambavyo vipengee tofautitofauti vya ushairi vinavyobainika. Aidha, wasomi hao wametafiti kuhusiana nanamna ya kufundisha ushairi. Japo tafiti nyingi zimefanywa kuhusiana na ushairi, pana haja kubwa ya kufanya utafiti kuhusiana na jinsi ya kufundisha mtindo katika ushairi. Hiki ndicho kichocheo cha makala hii. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu iliyoasisiwa na Boasna kuendelezwa naye Bakhtin. Nadharia hii ina mihimili kadhaa lakini mhimiliunaoshikilia kuwa tanzu huibua muundo wa kazi fulani ya fasihi na kufanya kazihiyo ieleweke kwa urahisi sana, ndio uliotumika katika utafiti huu.Utafiti huu ulitumia sampuli ya utabakishaji kuteua shule zilizoshiriki utafiti huu. Sampuli ya kimakusudi ilitumiwa kuteua walimu kwa sababu hao ndio walio na mamlaka ya kufundisha. Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini ina shule thelathini (30), hivyo basi utafiti ulizingatia asilimia thelathini (30%) kwa kuteua shule tisa (9). Utafiti huu ulitumia mbinu ya usaili nambinu ya uchunzaji kukusanya data zilizohitajika.Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa walimu walitumia maigizo, maswalina majibu, kazimradi, majadiliano, vikundi vya majadiliano, kanda au santuri, kukariri, kinuruweo na maelezo kama mbinu za ufundishaji kufundishia mtindo katika ushairi.Utafiti huu unapendekeza kuwawalimu wa Kiswahili watilie maanani mbinu mahususi wanapofundisha ushairi ili wanafunzi wachangamkie somo la ushairi. Vilevile, unapendekeza kuwa taasisi zinazokuza mitaala ziweze kuzingatia pakubwa sana mbinu mahususi ambazo zitatumiwa na walimu kwa ajili ya kuboresha zaidi ufundishaji wa ushairi. Aidha, unapendekeza kuwa tafiti nyingine zifanywe kuhusiana na jinsi ya kufundisha vipengee vingine vya ushairi kando na mtindo.