dc.description.abstract | Lugha ni chombo cha mawasiliano ambacho hakiwezi kuepukika katika uwanja wowote
ule palipo na maongezi hasa mahubiri. Lugha na dini vina historia ndefu kimahusiano hasa
tunaporejelea umuhimu na uarnilifu wa lugha katika bibilia. Kwa upande mwengine lugha
kitamathali imechukuliwa kuwa ya kimsingi sana katika dini. Hii ni kwa sababu, lugha
tamathali ni lugha atharishi ambayo huathiri hisia za watu, huingia katika fikra zao na
kuchochea mawazo yao. Miongoni mwa tamathali mbalimbali zikiwemo vinyume,
methali, isitiara na nyinginezo, sitiari na tashbiha zina uwezo na kipawa cha kisaikolojia
kinachoashiria undani na uimarishaji wa mawasiliano. Hiki ndicho kichocheo
kinachowasukuma wanafalsafa na wanauchanganuzi wa semi kuchanganua dhima ya lugha
ya kidini kama mbinu ya mawasiliano.
Kwa rnisingi hii utafiti huu unalenga maturnizi ya lugha ya kitamathali katika mahubiri ya
dini ya kikristu ambapo sitiari na tashbiha ndizo msingi wa utafiti huu. Malengo yake
maalum yanahusu; kufafanua rnisingi ya lugha tamathali husika kwa rnielekeo ya
wanafalsafa mbalimbali, ubainishaji wa sitiari na tashbiha zinazojitokeza katika mahubiri
ya dini ya kikristu katika Kiswahili, kuchanganua maana yake kiuarnilifu na kiuamalifu na
mwishowe kutathrnini thamani ya rnielekeo hii ya lugha katika mawasiliano ya dini.
Matumizi ya sitiari na tashbiha, na fasiri yake inahusu hasa mazingira ya muktadha na kwa
hivyo nadharia za kiuamali ni mielekeo mwafaka tuliyoitumia katika uchanganuzi wa
ithibati.
Kupitia mbinu za unasaji na ushiriki-utazamaji, katika makanisa ya rniji mikuii mmne
nchini Kenya, tulikusanya badhi ya sitiari na tashbiha zinazoturniwa katika mahubiri na
kuzichanganua kiuamali, kwa kukadiria maana yake mbali mbali, kisha kuonyesha
uamalifu na uarnilifu wa vitendo vitamkwa katika kufikia malengo yaliyonuiwa na
mhubiri. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa wahubiri huwasilisha uwanja mkubwa wa
kufasiria maana mbalimbali ya tamathali husika. Uthibiti wa .maana lengwa hutokana na
ushirika wa kimaana kwenye rnisingi ya imani za washirki. | en_US |