Maseno University Repository

Matumizi ya ngeli miongoni mwa wanafunzi wa kiswahili wa chuo kikuu cha Maseno, nchini Kenya

Show simple item record

dc.contributor.author LUKAMIKA , MaryKibigo
dc.date.accessioned 2019-01-18T12:16:00Z
dc.date.available 2019-01-18T12:16:00Z
dc.date.issued 2015
dc.identifier.uri https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/969
dc.description Masters Thesis en_US
dc.description.abstract Utafiti huu unachunguza matumizi ya ngeli miongoni mwa wanafunzi wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Maseno. Sura ya kwanza imeshughulikia ngeli kama msingi muhimu wa usarufi wa lugha za KiBantu hususan lugha ya Kiswahili. Dhana ya ngeli ni pana na tata kiasi cha kuwakanganya watumizi wengi wa Kiswahili wakiwemo wanafunzi. Mtazamo huu umechochewa na mkondo wa fikra unaotambua ngeli kama mojawapo ya vipengele muhimu vya sarufi ya Kiswahili. Licha ya kutekeleza wajibu huu, bado kuna ngeli ambazo hutatiza na kuzua changamoto kwa watumizi wa Kiswahili hasa wanafunzi, pengo ambalo utafiti huu unadhamiria kuliziba. Madhumuni mahsusi yalikuwa: Kubaini makosa yanayotokea wanafunzi wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Maseno wanapotumia ngeli, kujadili changamoto zinazotokea wanafunzi wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Maseno wanapotumia ngeli, na kupendekeza mikakati ya kukabiliana na matatizo hayo ya kisarufi na kuweza kuinua umilisi wa kiisimu katika Kiswahili miongoni mwao. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Makosa kulingana na Corder (1974). Mihimili mitano ya nadharia iliyotumiwa ni; Kukusanya sampuli ya lugha ya wanafunzi, kutambua, kuainisha, kuelezea na kutathmini makosa.Sura ya pili imefafanua tahakiki ya maandishi.Sura ya tatu imejikita katika kufafanua muundo mseto wa kitathmini na kitakwimu na njia na mbinu za utafiti zilizohusu uchunguzi maktabani na nyanjani. Ukusanyaji data nyanjani ulifanywa Kwa kuwarekodi wanafunzi wakijadiliana katika vikundi maalum vya Kiswahili kuhusu mada za kozi zinazohusu ngeli, kurekodi usaili pamoja na kuwapa mada za insha kuandikia na kuzisahihisha ili kupata data, baina ya mwezi wa Februari na Aprili, 2013. Uthibitishaji na uhakikishaji wa vifaa ulifanyiwa majaribio awali na wataalam katika Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika pamoja na utafiti wa awali. Usampulishaji mahuluti ulitumiwa ambapo uteuzi sampuli wa mtabakisho, uteuzi sahili usioratibiwa na usampulishaji maksudi zilitumiwa kuwateua wanafunzi 54 wa Kiswahili wanaochukua shahada ya kwanza kutoka kwa idadi ya jumla ya wanafunzi 540 kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa nne. Sura ya nne imeshughulikia uchanganuzi wa data uliojikita katika kusikiza na kunukuu rekodi za majadiliano na usaili na kuchanganua insha zilizoandikwa na kusahihishwa ili kulifikia lengo. Aidha, data zilichanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo na kijedwali. Utafiti huu umeonyesha bayana kuwa ngeli ni kipengele muhimu cha sarufi kinachodhihirisha umilisi na utendaji wa kiisimu katika lugha ya Kiswahili. Vilevile, utafiti umebaini ngeli za ziada na zinazotatiza hususan LI-YA, PA-KU-MU na KI-VI pamoja na changamoto zake zinazohusu vivumishi tata kama, jingine na lingine; zingine na nyingine katika ngeli za LI-YA na I-ZI mtawalia. Mikakati kama uzingativu wa maana na sarufi ilipendekezwa, ili kukabiliana na matatizo hayo ya sarufi na kuinua umilisi wa kiisimu katika Kiswahili miongoni mwao. Uchunguzi huu uliuwezesha utafiti kufikia malengo yake na kujibu maswali yote ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yalikusudia kutoa mwanga zaidi uelewa wa matumizi ya ngeli katika Chuo Kikuu cha Maseno, Vyuo Vikuu na lugha ya Kiswahili kwa jumla. Hata hivyo, utafiti huu ulidhihirisha kuwa dhana ya ngeli bado ilikuwa tatizo kwa wanafunzi wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Maseno hasa wa viwango vya chini kwani baadhi yao hawakuelewa msingi wake. Kwa hivyo, utafiti huu unapendekeza kuwa kuna haja ya dharura kwa wapangaji sera wa Kiswahili kuandaa semina, warsha na kongamano ili kuhamasisha wanafunzi wa Kiswahili kuhusu umuhimu wa dhana ya ngeli katika Chuo Kikuu cha Maseno, lugha ya Kiswahili na isimu kwa jumla. en_US
dc.language.iso en_US en_US
dc.publisher Maseno University en_US
dc.subject Kiswahili en_US
dc.title Matumizi ya ngeli miongoni mwa wanafunzi wa kiswahili wa chuo kikuu cha Maseno, nchini Kenya en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Maseno University Repository


Browse

My Account