dc.description.abstract | Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu huo katika kujifunza ushairi wa Kiswahili.Ugumu katika ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili umesababisha matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa katika somo la ushairi wa Kiswahili nchini Uganda.Hata hivyo ushairi wa Kiganda umekuwa unafanywa vizuri katika mtihani wa kitaifa. Wanafunzi hawa wanasomea katika mandhari sawa, utafiti huu ulichunguza kwa nini wanafunzi wanaofanya mtihani wa ushairi wa Kiganda wanatenda vizuri kuliko wanafunzi wa ushairi wa Kiswahili. Kwa hivyo utafiti huu ulichanganua mchango wa ushairi wa Kiganda katika kuendeleza umitindo wa ushairi wa Kiswahili, mfano wa ufundishaji wa ushairi katika wilaya ya mukono-nchini Uganda.Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa: Kufafanua jinsi muundo wa ushairi wa Kiganda unavyoweza kuendeleza muundo wa ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji.Kudadavua jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kusahilisha mtindo katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji na kutathimini jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kukuza maudhui katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya umitindo yaViktor Shklovsky (1904) na kuelezwa na Mbatia (2001) katika muktadha wa Kiswahili na umuundo ambayo iliasisiwa na Ferdinard de Saussure (1909) na Ntarangwi (2004), mihimili ya nadharia hii ni: Fasihi inastahili kuchunguzwa kama muundo mmoja uliojengwa kwa vipengele tofauti vinavyoshirikiana kukiunda kitu kizima. Pili huchunguza vipengele mbalimbali vya mfumo wa fasihi kwa kuchunguza jinsi vinavyohusiana na kuchangiana katika kukamilisha kazi husika. Tatu hulenga maana katika matini ya kifasihi na kupuuza maswala mengine ya nje kama muktadha. Utafiti huu ulitumia muundo elezi na data za utafiti huu zilichambuliwa kithamano. Mashairi yalikusanywa kutoka diwani mbili za Kiswahili na mbili za Kiganda. Mashairi 60 yalikusanywa yaani 30 ya Kiganda na 30 ya Kiswahili na 15 yalichaguliwa kutoka kila lugha kwa kutumia uteuzi nasibu. Mashairi yalitolewa kwenye diwani za Kiswahili; Malenga wa ziwa kuu ya Wallah bin Wallah naSauti ya dhikiya Abdilatif Abdalla na za Kiganda; Ab’Oluganda ab’Enda emu ya Hugo Sematimbana Balya n’ensekeezi ya Masagazi K. Vilichaguliwa kwa kuwa viko kwenye silabasi. Kundi lengwa ni Walimu watano wa Kiganda na watano wa Kiswahili ambao walichaguliwa kimakusudi na kushiriki katika uchambuzi ambao uliandamana na maoni yao kuhusu ujifunzaji na ufunzaji wa ushairi. Mashairi yalianishwa na ya Kiganda yalitafsiriwa kwa Kiswahili. Data ilikusanywa kwa kutumia simu kunasa sauti. Mashairi yalinukuliwa, yalitafsiriwa, na kisha kuchambuliwa kimuundo, kimtindo na kimaudhui. Data za utafiti huu ziliwasilishwa kwa mfumo wa kinathari. Utafiti huu ulikuwa utafiti wa nyanjani na maktabani, ulifanyiwa katika wilaya ya Mukono. Shule tano zilitumiwa kati ya shule ishirini zinazofunza Kiswahili, ziliteuliwa kimakusudi kwa kuwa zinafundisha Kiswahili na Kiganda kwenye kiwango cha A kisha uchanganuzi wa data ulifanywa kithamano na data kuwasilishwa kwa mjadala. Utafiti huu uligundua kuwa ushairi wa Kiswahili waweza kukopa vipengele vya muundo, mtindo, na maudhui vya ushairi wa Kiganda na kuviendeleza vipengele hivi katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulifafanua jinsi mwalimu wa ushairi wa Kiswahili anavyoweza kuhamisha maarifa kutoka ushairi wa Kiganda hadi wa Kiswahili. Utasaidia kuendeleza ushairi wa Kiswahili kuhamisha maarifa ya ujifunzaji na ufunzaji kutokana na ushairi wa Kiganda ili kusahilisha ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili na kuuendeleza. | en_US |