Show simple item record

dc.contributor.authorOgonda S Sinzore, Deborah N Amukowa, Beverlyne A Ambuyo
dc.date.accessioned2022-10-16T13:27:16Z
dc.date.available2022-10-16T13:27:16Z
dc.date.issued2021
dc.identifier.urihttps://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5416
dc.description.abstractTafiti nyingi zilizofanywa kumhusu mhusika mwanamke katika tamthilia za Kiswahili zilimsawiri mwanamke kwa ujumla bila kuangazia uongozi wake. Chache zilizoshughulikia mwanamke kiongozi zimefanya hivi bila kuangazia mitindo ya lugha inayochangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi. Mitindo ya lugha ni muhimu katika kuibua maudhui ya kazi ya fasihi. Makala hii ililenga kuchanganua mitindo ya lugha inayomsawiri mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango (Wamitila, 2003) na Kigogo (Kea, 2016). Zimelengwa tamthilia hizi kwa kuwa zimeandikwa baada ya mwaka 2000 ambapo hadhi ya mwanamke kiongozi imeendelea kuimarika na jamii kuonekana kukubali uongozi wa mwanamke. Tamthilia za Pango na Kigogo ziliteuliwa kupitia mbinu ya usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zina wahusika wanawake ambao ni viongozi. Nadharia ya Udenguzi iliyoasisiwa na Derrida (1966) na kuelezwa na Ntarangwi (2004) iliteuliwa kwa ajili ya utafiti huu. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo (maudhui) ilitumiwa kukusanya data. Tamthilia teule zilisomwa na data kunukuliwa. Data ilipangwa kisha ikachanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kupitia makala hii kuwa mitindo mbalimbali ya lugha imechangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango na Kigogo.en_US
dc.publisherUniversity of Dar es salaamen_US
dc.titleMitindo ya Lugha Inayomsawiri Mwanamke Kiongozi katika Tamthilia za Pango (2003) na Kigogo (2016)en_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record