dc.contributor.author | Mulei Martin, Debora Nanyama, Beverlyne Ambuyo | |
dc.date.accessioned | 2022-10-16T13:13:05Z | |
dc.date.available | 2022-10-16T13:13:05Z | |
dc.date.issued | 2021 | |
dc.identifier.issn | 2707-3467(Print),2707-3475(Online) | |
dc.identifier.uri | https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5415 | |
dc.description | https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.331 | en_US |
dc.description.abstract | Makala hii inaonesha athari za kimofosintaksia za ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Makala hii inatokana na kuwa, Luganda na Kiswahili huainisha ngeli kutumia mfumo mmoja na matumizi yake kuzingatia sheria za kuonyesha upatanishi wa kisarufi wa nomino na maneno mengine katika tungo kimofosintaksia. Uwiano na tofauti za kanuni za matumizi ya vipashio vya kimofosintaksia baina ya lugha asili na Kiswahili sanifu umeripotiwa kuingiliana na kuathiri matumizi ya Kiswahili sanifu. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa maandishi na mazungumzo ya wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Luganda na ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya pili ulikiuka utaratibu wa kisarufi wa matumizi ya Kiswahili sanifu. Data ilitokana na uchanganuzi wa maandishi na mazungumzo ya wanafunzi 117, usaili na mijadala ya walimu 30 kutoka shule za upili 15 teule, wilayani Kampala, Uganda. Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya sarufi bia na upatanifu wa nadharia ya Umilikifu na unganifu (Chomsky, 1981) ambayo huonesha ubia wa lugha na hali ya vipashio fulani vya kisarufi kutawala vipashio vingine katika tungo. Matokeo ya tathmini ya kanuni za matumizi ya kipashio cha kimofosintaksia cha ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu yalidhihirisha athari za; uhamishaji wa maumbo, mofofonolojia, ubebaji wa viambishi vya ngeli tofauti, uchopekaji wa viambishi, ubadilishanaji wa viambishi ngeli, uchanganyaji wa maumbo na ujumlishaji wa viambishi vya msingi vya ngeli ya Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Makala hii inatarajiwa kuwasaidia walimu na wanafunzi kutambua athari za lugha ya kwanza katika matumizi ya Kiswahili sanifu, kuweka mikakati ya kuondokana na athari hizi kujenga matumizi bora ya Kiswahili sanifu. | en_US |
dc.publisher | Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili | en_US |
dc.title | Athari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wanafunzi Shuleni, Uganda | en_US |
dc.type | Article | en_US |