Maseno University Repository

UCHANGANUZI WA HIPONIMIA ZA VITENZI VYA KISWAHILI.

Show simple item record

dc.contributor.author Benard Odoyo Okal, Florence Indede, Ernest Sangai Mohochi
dc.date.accessioned 2020-11-30T08:18:13Z
dc.date.available 2020-11-30T08:18:13Z
dc.date.issued 2016
dc.identifier.uri https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/3068
dc.description.abstract Hiponimia ni uhusiano wa kifahiwa unaodhihirika baina ya leksimu ya jumla (hipanimu) na mahususi (hiponimu). Kama vile hipanimu mzazi hujumuisha hiponimu baba na mama. Uhusiano huu wa kihi-ponimia ulidhukuriwa na wanaisimu wa awali kuwa unahusisha leksimu nomino pekee. Hata hivyo, tafiti za hivi punde zinadhihirisha kuwa hiponimia huweza kudhihirika pia miongoni mwa kategoria za vivumishi, vielezi na vitenzi. Ingawa kuna midhihiriko ya hiponimia za vitenzi vya Kiswahili, wataa-lamu kadha wameelekea kushughulikia hiponimia za nomino na kutotilia maanani vitenzi. Hivyo basi, makala hii imechanganua uhusiano wa kihiponimia unaodhihirika miongoni mwa vitenzi teule vya Kiswahili. Katika kushughulikia suala hili, hipanimu vitenzi 24 kutoka kamusi za Kiswahili zimeteuli-wa kimakusudi na hiponimu husika kutolewa. Nadharia ya Uchanganuzi Vijenzi kwa mujibu wa Katz na Fodor imezingatiwa katika uchanganuzi wa hiponimia hizi. Katika nadharia hii, sifa bainifu za hiponimu husika huonyeshwa kwa kutumia alama maalum za [+, -]. Data kuhusu hiponimia za vitenzi ilipekuliwa kutoka kamusi za Kiswahili kwa kuzingatia mwelekeo wa kiishara au kisintaksia kwa mujibu wa Hearst, na Snow na wenzake ili kuweza kutambua hipanimu na hiponimu husika katika sentensi. Hiponimia hizi zimechanganuliwa na kuwasilishwa kwa mtindo wa nadharia ya seti. en_US
dc.publisher Swahili Forum en_US
dc.title UCHANGANUZI WA HIPONIMIA ZA VITENZI VYA KISWAHILI. en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Maseno University Repository


Browse

My Account