Department of Kiswahili & Other African Languages
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/105
2024-03-29T10:16:03ZMitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5841
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Odhong’, Joseph Ondiek; Amukowa, Debora Nanyama; Asiko, Beverlyne Ambuyo
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi mazingira wanamoishi. Tangu jadi wahakiki wamejitahidi kueleza vipi wahusika wazimu wametumika katika fasihi. Tahakiki za tamthilia za Shakespeare na za Kiingereza za karne ya ishirini zimeeleza namna na sababu za uumbaji wao. Katika riwaya za Kiswahili hakuna tahakiki zinazoshughulikia wahusika wazimu wala mitindo ya lugha inayowabainisha. Makala hii ilidhamiria kuchanganua mitindo ya lugha inayowabainisha wahusika wazimu katika kazi teule za Habwe. Uteuzi huu ulitokana na Habwe kusifiwa kuwa mwandishi wa fasihi ya kiongofu aliyetumia motifu ya wazimu katika riwaya zake (Gromov, 2018). Riwaya tano za Habwe: Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008), Fumbo La Maisha (2009), Safari ya Lamu (2011) na Kovu Moyoni (2014) ziliteuliwa kupitia usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zilikuwa na wahusika wazimu. Nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Bally (1909) ) na kuendelezwa na Thornborrow na Wareing (1998) iliteuliwa kwa ajili ya kazi hii. Muundo wa kiuchanganuzi umetumiwa. Data zilikusanywa kutumia kifaa cha kudondoa data kilichokuwa na vidokezo vya mitindo ya lugha inayotambulisha wahusika wazimu. Matini ya riwaya teule imesomwa kwa makini na vipengele mbalimbali, kurekodiwa. Kisha data imechanganuliwa, kufasiriwa na kuratibiwa kulingana na madhumuni ya utafiti. Matokeo yamewasillishwa kwa njia ya maelezo. Makala hii imedhihirisha jinsi mitindo ya lugha ilivyotumiwa kuwatambulisha wahusika wazimu.
https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1345
2023-07-31T00:00:00ZNafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5673
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Barasa Martin Mulwale, Ngesa Florence Indede, Asiko Beverlyne Ambuyo
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufahamu na kutagusana na ulimwengu huhitaji matumizi ya kiisimu ya kipekee. Katika muktadha wa kidini kuna changamoto ya asili ya maneno, mamlaka, utambulisho na ushirikiano wa wahusika. Aidha, miktadha mbalimbali ya kidini hutumia lugha kutimiza mahitaji yake maalum. Lugha hutenda matendo, huomba maombi ya kukemea, husimulia hali za kijamii na hata huonekana kudhibiti matendo ya Maulana. Ni kwa misingi hii ndipo kazi hii inajukumika kutalii jinsi lugha ya Kiswahili na Kibukusu zinavyotagusana katika mawanda haya ya dini, hasa Dini ya Musambwa (DYM) ambayo inaaminika kuwa ya kiasili katika jamii hii ya Wabukusu katika Kaunti ya Bungoma. Kazi hii inazingatia misingi ya Spolsky (2004, 2006, 2009) ambaye anajadili kuwa sera ya lugha halisi ya jamii hupatikana kwenye matumizi yake. Anazingatia Mwelekeo wa ikolojia ya lugha uliozinduliwa na Haugen (1972) unaochunguza mwingiliano baina ya lugha na mazingira. Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Kupitia uchunzaji wa kutoshiriki moja kwa moja mtafiti alihudhuria ibada na kunasa mazungumzo yao kwenye kanda ya kunasia sauti. Mazungumzo hayo yalinakiliwa na orodha ya uchunzaji ilitumiwa kubainisha na kueleza namna lugha ya Kibukusu na Kiswahili zilivyotumiwa katika shughuli za kanisa hilo. Hali ya kuchanganya na kubadili msimbo, utohozi na hata matumizi ya Kiswahili kwa Kibukusu haikuweza kuepukika. Utafiti huu unadhihirisha kuwa raslimali za lugha zilizopo katika ikolojia fulani huchagizana katika kukamilisha majukumu ya mawasiliano katika muktadha husika.
DOI: https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1147
2023-03-27T00:00:00ZKubainisha Usawiri wa Ukahaba naWahusika Makahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5672
Kubainisha Usawiri wa Ukahaba naWahusika Makahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi
Karuhanga Deusdedit, Indede Florence, Nanyama Deborah Amukowa
Utafiti huu ulichunguza ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia. Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile TalcortParsons na EmileDurkheim kama wanavyonukuliwa na WorselyIntroductiontoSociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki. Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na FredrichEngles(1820-1895). Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi. Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu. Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Kimataifa Metropolitan, na maktabani ya shule ya upili Heritage. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano. Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki. Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi
DOI: https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.1005
2022-12-28T00:00:00ZPhonemic Representation and Transcription for Speech to Text Applications for Under-resourced Indigenous African Languages: The Case of Kiswahili
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5499
Phonemic Representation and Transcription for Speech to Text Applications for Under-resourced Indigenous African Languages: The Case of Kiswahili
Awino, Ebbie ; Wanzare, Lilian; Muchemi, Lawrence ; Wanjawa, Barack ; Ombui, Edward ; Indede, Florence ; McOnyango, Owen ; Okal, Benard
Building automatic speech recognition (ASR) systems is a challenging task, especially for under resourced languages that need to construct corpora nearly from scratch and lack sufficient training
data. It has emerged that several African indigenous languages, including Kiswahili, are technologically
under-resourced. ASR systems are crucial, particularly for the hearing-impaired persons who can
benefit from having transcripts in their native languages. However, the absence of transcribed speech
datasets has complicated efforts to develop ASR models for these indigenous languages. This paper
explores the transcription process and the development of a Kiswahili speech corpus, which includes
both read-out texts and spontaneous speech data from native Kiswahili speakers. The study also
discusses the vowels and consonants in Kiswahili and provides an updated Kiswahili phoneme
dictionary for the ASR model that was created using the CMU Sphinx speech recognition toolbox, an
open-source speech recognition toolkit. The ASR model was trained using an extended phonetic set
that yielded a WER and SER of 18.87% and 49.5%, respectively, an improved performance than
previous similar research for under-resourced languages.
2022-01-01T00:00:00ZMitindo ya Lugha Inayomsawiri Mwanamke Kiongozi katika Tamthilia za Pango (2003) na Kigogo (2016)
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5416
Mitindo ya Lugha Inayomsawiri Mwanamke Kiongozi katika Tamthilia za Pango (2003) na Kigogo (2016)
Ogonda S Sinzore, Deborah N Amukowa, Beverlyne A Ambuyo
Tafiti nyingi zilizofanywa kumhusu mhusika mwanamke katika tamthilia za Kiswahili zilimsawiri mwanamke kwa ujumla bila kuangazia uongozi wake. Chache zilizoshughulikia mwanamke kiongozi zimefanya hivi bila kuangazia mitindo ya lugha inayochangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi. Mitindo ya lugha ni muhimu katika kuibua maudhui ya kazi ya fasihi. Makala hii ililenga kuchanganua mitindo ya lugha inayomsawiri mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango (Wamitila, 2003) na Kigogo (Kea, 2016). Zimelengwa tamthilia hizi kwa kuwa zimeandikwa baada ya mwaka 2000 ambapo hadhi ya mwanamke kiongozi imeendelea kuimarika na jamii kuonekana kukubali uongozi wa mwanamke. Tamthilia za Pango na Kigogo ziliteuliwa kupitia mbinu ya usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zina wahusika wanawake ambao ni viongozi. Nadharia ya Udenguzi iliyoasisiwa na Derrida (1966) na kuelezwa na Ntarangwi (2004) iliteuliwa kwa ajili ya utafiti huu. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo (maudhui) ilitumiwa kukusanya data. Tamthilia teule zilisomwa na data kunukuliwa. Data ilipangwa kisha ikachanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kupitia makala hii kuwa mitindo mbalimbali ya lugha imechangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango na Kigogo.
2021-01-01T00:00:00ZAthari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wanafunzi Shuleni, Uganda
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5415
Athari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wanafunzi Shuleni, Uganda
Mulei Martin, Debora Nanyama, Beverlyne Ambuyo
Makala hii inaonesha athari za kimofosintaksia za ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Makala hii inatokana na kuwa, Luganda na Kiswahili huainisha ngeli kutumia mfumo mmoja na matumizi yake kuzingatia sheria za kuonyesha upatanishi wa kisarufi wa nomino na maneno mengine katika tungo kimofosintaksia. Uwiano na tofauti za kanuni za matumizi ya vipashio vya kimofosintaksia baina ya lugha asili na Kiswahili sanifu umeripotiwa kuingiliana na kuathiri matumizi ya Kiswahili sanifu. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa maandishi na mazungumzo ya wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Luganda na ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya pili ulikiuka utaratibu wa kisarufi wa matumizi ya Kiswahili sanifu. Data ilitokana na uchanganuzi wa maandishi na mazungumzo ya wanafunzi 117, usaili na mijadala ya walimu 30 kutoka shule za upili 15 teule, wilayani Kampala, Uganda. Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya sarufi bia na upatanifu wa nadharia ya Umilikifu na unganifu (Chomsky, 1981) ambayo huonesha ubia wa lugha na hali ya vipashio fulani vya kisarufi kutawala vipashio vingine katika tungo. Matokeo ya tathmini ya kanuni za matumizi ya kipashio cha kimofosintaksia cha ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu yalidhihirisha athari za; uhamishaji wa maumbo, mofofonolojia, ubebaji wa viambishi vya ngeli tofauti, uchopekaji wa viambishi, ubadilishanaji wa viambishi ngeli, uchanganyaji wa maumbo na ujumlishaji wa viambishi vya msingi vya ngeli ya Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Makala hii inatarajiwa kuwasaidia walimu na wanafunzi kutambua athari za lugha ya kwanza katika matumizi ya Kiswahili sanifu, kuweka mikakati ya kuondokana na athari hizi kujenga matumizi bora ya Kiswahili sanifu.
https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.331
2021-01-01T00:00:00ZUamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5414
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Mulwale, Barasa, Ngesa, Florence, Indede, Asiko,Beverlyne Ambuyo
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi yoyote ile. Nchini Kenya, vipengele katika katiba ya 2010, vinavyohusu lugha vilipandisha hadhi lugha ya Kiswahili ili iweze kutumika kama lugha ya taifa na rasmi sambamba na Kiingereza. Hata hivyo, katiba hii haijaweka kanuni zinazolenga kuimarisha na kudumisha uanuwai wa lugha za kiasili kote nchini Kenya. Machukulio ni kwamba, vipengele vya katiba vinasheheni sifa stahilifu kama vile, usawa wa kimatumizi, utekelezwaji, mikao ya kieneo, matakwa, pamoja na hiari za wananchi. Kwa kuangazia hali ya kiisimu-jamii katika Kaunti ya Bungoma, utata upo katika udumishaji wa mfumo ‘rasmi’ wa sera ya lugha Kitaifa, na utekelezwaji wa sera ya lugha kupitia asasi za serikali na zile za umma. Kazi hii inalenga kuchanganua uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu kupitia ruwaza zinazodhihirika katika mawanda mbalimbali ya lugha katika Kaunti ya Bungoma. Mihimili ya nadharia ya sera ya lugha iliyoendelezwa na Spolsky (2004, 2007) ambayo ni Usimamizi wa lugha na Ikolojia ya lugha pamoja na ruwaza za lugha ilivyoelezwa na Paltridge (2001) ndiyo nguzo ya kuchanganua utafiti huu. Aidha, mtazamo wa Haugen (1972) unaohusu Ikolojia ya lugha umetumika katika kudhihirisha michakato baina ya lugha na mazingira inamotumika. Muundo mseto uliojumuisha, muundo wa kimaelezo, kiupelelezi na wa kiiktisadi ulitumiwa. Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kuteua matumizi ya lugha ya KS, KB na KS/KB katika ruwaza za lugha zilizodhihirika katika mawanda ya biashara, kanisani na utawala hasa kwenye mikutano ya umma au baraza za Chifu katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Bungoma. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchunzaji usio-shirikishi na ya kiiktisadi ilikusanywa kwa kuhesabu hali ambazo lugha za KS, KB au KS/KB zilitumiwa. Ilibainika kuwa lugha ya KS na KB hukamilishana kiuamilifu katika mawanda mbalimbali ya kijamii katika Kaunti ya Bungoma.
DOI: https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.665
2022-01-01T00:00:00ZKenSwQuAD--A Question Answering Dataset for Swahili Low Resource Language
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/5282
KenSwQuAD--A Question Answering Dataset for Swahili Low Resource Language
Barack Wanjawa, Lilian Wanzare, Florence Indede, Owen McOnyango, Lawrence Muchemi, Edward Ombui
This research developed a Kencorpus Swahili Question Answering Dataset KenSwQuAD from
raw data of Swahili language, which is a low resource language predominantly spoken in
Eastern African and also has speakers in other parts of the world. Question Answering
datasets are important for machine comprehension of natural language processing tasks such
as internet search and dialog systems. However, before such machine learning systems can
perform these tasks, they need training data such as the gold standard Question Answering
(QA) set that is developed in this research. The research engaged annotators to formulate
question answer pairs from Swahili texts that had been collected by the Kencorpus project, a
Kenyan languages corpus that collected data from three Kenyan languages. The total Swahili
data collection had 2,585 texts, out of which we annotated 1,445 story texts with at least 5
QA pairs each, resulting into a final dataset of 7,526 QA pairs. A quality assurance set of 12.5%
of the annotated texts was subjected to re-evaluation by different annotators who confirmed
that the QA pairs were all correctly annotated. A proof of concept on applying the set to
machine learning on the question answering task confirmed that the dataset can be used for
such practical tasks. The research therefore developed KenSwQuAD, a question-answer
dataset for Swahili that is useful to the natural language processing community who need
training and gold standard sets for their machine learning applications. The research also
contributed to the resourcing of the Swahili language which is important for communication
around the globe. Updating this set and providing similar sets for other low resource
languages is an important research area that is worthy of further research.
https://doi.org/10.48550/arXiv.2205.02364
2022-01-01T00:00:00ZJinsi Mtindo Katika Ushairi Unavyofundishwa Katika Shule za Upili: Mfano wa Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini, Kaunti ya Busia, Kenya
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/4889
Jinsi Mtindo Katika Ushairi Unavyofundishwa Katika Shule za Upili: Mfano wa Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini, Kaunti ya Busia, Kenya
9. Mukoya, H., Wasike, M., Amukowa, D., & Masinde, E
Makala hii inahusu jinsi ambavyo mtindo katika ushairi unavyofundishwa katika shule za upili nchini Kenya. Wasomi mbalimbali wametafiti kuhusiana na jinsi ambavyo vipengee tofautitofauti vya ushairi vinavyobainika. Aidha, wasomi hao wametafiti kuhusiana nanamna ya kufundisha ushairi. Japo tafiti nyingi zimefanywa kuhusiana na ushairi, pana haja kubwa ya kufanya utafiti kuhusiana na jinsi ya kufundisha mtindo katika ushairi. Hiki ndicho kichocheo cha makala hii. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utanzu iliyoasisiwa na Boasna kuendelezwa naye Bakhtin. Nadharia hii ina mihimili kadhaa lakini mhimiliunaoshikilia kuwa tanzu huibua muundo wa kazi fulani ya fasihi na kufanya kazihiyo ieleweke kwa urahisi sana, ndio uliotumika katika utafiti huu.Utafiti huu ulitumia sampuli ya utabakishaji kuteua shule zilizoshiriki utafiti huu. Sampuli ya kimakusudi ilitumiwa kuteua walimu kwa sababu hao ndio walio na mamlaka ya kufundisha. Kaunti Ndogo ya Teso Kaskazini ina shule thelathini (30), hivyo basi utafiti ulizingatia asilimia thelathini (30%) kwa kuteua shule tisa (9). Utafiti huu ulitumia mbinu ya usaili nambinu ya uchunzaji kukusanya data zilizohitajika.Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa walimu walitumia maigizo, maswalina majibu, kazimradi, majadiliano, vikundi vya majadiliano, kanda au santuri, kukariri, kinuruweo na maelezo kama mbinu za ufundishaji kufundishia mtindo katika ushairi.Utafiti huu unapendekeza kuwawalimu wa Kiswahili watilie maanani mbinu mahususi wanapofundisha ushairi ili wanafunzi wachangamkie somo la ushairi. Vilevile, unapendekeza kuwa taasisi zinazokuza mitaala ziweze kuzingatia pakubwa sana mbinu mahususi ambazo zitatumiwa na walimu kwa ajili ya kuboresha zaidi ufundishaji wa ushairi. Aidha, unapendekeza kuwa tafiti nyingine zifanywe kuhusiana na jinsi ya kufundisha vipengee vingine vya ushairi kando na mtindo.
2019-01-01T00:00:00ZMatumizi ya Maigizo Kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia Katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenya
https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/4888
Matumizi ya Maigizo Kama Mbinu ya Kufundisha Tamthilia Katika Shule za Upili, Kaunti ya Bungoma Kusini, Kenya
8. Simbi, I., Wasike, M., Amukowa, D., & Masinde, E
Utafiti huu ulilenga kuonyesha matumizi ya maigizo kama mbinu ya kufundisha
tamthilia; mfano wa Kigogo katika shule za upili, Kaunti ya Bungoma Kusini.
Ufundishaji wa somo lolote hujikita kwenye mawasiliano baina ya mwalimu na
mwanafunzi. Mbinu za kufundisha huwa viungo muhimu vya kufanikisha
mawasiliano haya. Mwalimu ana jukumu la kuteua mbinu mwafaka ya
kufundisha. Kuna mbinu mbalimbali mwalimu anaweza kutumia kufundisha
tamthilia. Utafiti huu umechagua maigizo kama mbinu ya kufundisha tamthilia.
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza iwapo walimu wanatumia mbinu ya
maigizo kufundisha tamthilia na wanatumia kwa jinsi gani. Utafiti huu
uliongozwa na nadharia ya utendaji inayoshikilia kuwa matini ya kidrama
huwasilisha ujumbe vyema zaidi kupitia uigizaji wake katika jukwaa. Utafiti
ulilenga shule kumi na sita kati ya shule hamsini na mbili. Walimu
wanaofundisha Kiswahili kidato cha tatu na nne pamoja na wanafunzi wa kidato
cha tatu na nne ndio waliolengwa. Watafitiwa waliteuliwa kwa kutumia mbinu
ya utabakishaji, kinasibu na usampulishaji kimaksudi. Stadi ya utabakishaji
ilitumika kuainisha shule katika makundi matatu. Mbinu ya kimaksudi ilitumika
kuteua shule tatu za kaunti na walimu wanaofundisha kiswahili kidato cha tatu
na nne. Mbinu ya kinasibu ilitumika kuteua shule za kaunti ndogo, shule kumi
na mbili na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Wanafunzi kumi katika kila
kidato waliteuliwa, jumla ya wanafunzi mia tatu ishirini walitafitiwa. mbinu
zlizotumika kukusanya data zilikuwa hojaji, maswali ya usaili na uchunzaji.
Maswali ya usaili yalitumika kukusanya data kutoka kwa walimu. Data
ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia maelezo, asilimia, picha na
majedwali. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa kuwa walimu 83% ndio walitumia
mbinu ya maigizo kufundisha tamthilia ya Kigogo. Utafiti unapendekeza kuwa
mbinu za maigizo ambazo hazitumiki pia zitumike ili kuboresha ufundishaji.
Vile vile taasisi ya elimu kuandaa semina na warsha za kuwahamasisha walimu
kuhusu njia mbalimbali za kutumia maigizo kufundisha. Aidha kila shule iwe
na klabu cha maigizo ili kutumika katika ufundishaji wakati wowote.
2019-01-01T00:00:00Z